登入選單
返回Google圖書搜尋
Kamusi ya Ukristo
註釋

Kamusi yoyote ni kazi ya maarifa, ni chemchemi ambayo maji yake hayakauki, hutiririsha maarifa na kuchochea watumiaji kutaka kuijua zaidi. Kamusi ya Ukristo inazo sifa hizi, na za ziada kwani ni kamusi ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili ambayo inaweka pamoja, tafsiri ya dhana mbalimbali, majina mbalimbali ya Wakristo na desturi za Makanisa ya Kikristo.

Kamusi ya Ukristo ni kamusi ambayo kwa umahili mkubwa mwandishi amefatilia na kufanikiwa kukusanya vitomeo vinavyowakilisha madhehebu mbalimbali ya Kikristo. Kuna vidahizo ambavyo hutumiwa zaidi na dhehebu moja kuliko lingine, lakini mwandishi ameviweka pamoja ili kuuondoa umadhehebu na kuujenga umoja wa Ukristo. Ni ukweli usiopingika kuwa waamini wengi hawaelewi misamiati na istilahi nyingi za dini zao. Hivyo basi kwa msaada wa Kamusi hii msomaji atafaidi maarifa ya maana na matumizi ya maneno si tu ya dhehebu moja, dhehebu lake, bali Ukristo kwa ujumla wake.

Kamusi ya Ukristo is the first dictionary in Swahili language which puts together the interpretation of various concepts, different names for Christians and customs of the Christian churches.